Rapa Nazizi aachia video ya kwanza ‘Gai Fafa’

NAIROBI: RAPA kutoka Kenya Nazizi amerejea kwenye ulingo wa muziki na wimbo mpya unaoitwa “Gai Fafa” baada ya kuwa nje ya muziki kwa muda mrefuu kutokana na masuala ya uzazi.
“Gai Fafa” ni wimbo wa kujisikia raha na lkuachana na mizigo ya maisha ya changamoto ya muda mrefu sasa ameamua kurudi na kufurahia maisha akisahau yote mabaya yaliyomfika.
Nazizi amesema wimbo na videwo hiyo ni zawadi kwa mashabiki wake na heshima kwa rafiki yake mpendwa. “Hii ni ya mashabiki ambao wamenichelewesha kwa miaka 25. Siwezi kueleza jinsi ujumbe na utiaji moyo ulivyonisaidia. Nilihitaji kusema asante kwa njia pekee ninayojua kupitia muziki. Na pia ni kwa ajili ya Hilton. Aliupenda wimbo huu sana na aliendelea kunisukuma kuuachia.”
Video ya muziki ilifanywa Arusha, Tanzania na director Okey, huku wacheza densi ikiwa ni kundi la Purple Dancers Crew wakiongozwa na Chiki na Kevo kutoka kundi la The Dance Shagz kutoka Kenya.
Anajulikana kama Mke wa Rais wa reggae na hip hop ya Kenya, Nazizi anaingia kwenye furaha na kusahau changamoto alizopitia kwa miaka mingi, “Yote ni kuhusu kuachilia mafadhaiko, kucheza kwa na kuwa na furaha hata kwa muda mfupi. “Hii ni video yangu ya kwanza kabisa inayotegemea dansi na ninafurahi kuona changamoto zimeondoka.”
“Gai Fafa” haijaunganishwa kwenye albamu; badala yake, ni kutolewa kwa ajili ya mashabiki wake tu wapate furaha ya msanii wao kurudi upya kabla hajaachia albamu yake mpya.
Wimbo huo uliimbwa moja kwa moja kwenye Blankets & Wine mnamo Desemba 2024, ambapo alizua hisia za wengi walioudhuria wakati alipouimba kwa mara ya kwanza.
Nazizi yupo mbioni kuachia EP yake yenye nyimbo sita za reggae baadaye mwaka huu akisema kwamba ni kwa ajili ya mashabiki wake wanaopenda muziki wa reggae.