Filamu
Rammy Galis afichua aliwahi kukaa gerezani kwa kusingiziwa

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Movie, Rammy Galis, amefunguka kuhusu tukio zito lililowahi kumpata katika maisha yake, akisema aliwahi kukaa gerezani kwa kipindi cha miezi 10 baada ya kusingiziwa.
Rammy ameeleza kuwa wakati huo alikuwa akifanya kazi katika shirika moja la benki, ambako ndipo matatizo hayo yalianzia.
“Nilifanya kazi kwenye shirika la benki nitaliweka hilo kwenye mabano. Nilipata matatizo nikiwa benki, nilipata kesi ya wizi wa fedha. Niliishtakiwa, siyo kuhukumiwa, lakini nilienda kukaa Keko miezi 10,” amesema Rammy.
Amesema kipindi hicho kilikuwa kigumu katika maisha yake, lakini kilimjenga na kumpa mtazamo mpya kuhusu maisha na watu.




