Rais wa Yanga X Rais wa Wanaume duniani

Rais wa Klabu ya Yanga Hersi Said leo amempokea Nyota wa Kimataifa wa Morocco anaekipiga PSG ya Ufaransa Archraf Hakimi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanajaro (KIA)
Hakimi yupo mapumzikoni ambapo atatumia muda wa wiki moja kushuhudia mazuri yalipo Tanzania.
Siku kadhaa nyuma Hersi na Hakimi walionekana pamoja nchini Ufaransa, na hapa labda ndio mipango ya safari hii ilipoanzia.
Ikumbukwe siku za hivi karibuni Hakimi alijizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni hasa kwa wanaume baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili dhidi ya aliyekuwa mke wake ambaye alifungua kesi ya talaka akidai nusu ya mali za nyota huyo.
Hakimi alishinda kesi hiyo baada ya kubainika hamiliki chochote kwani mali zote ameziandika kwa jina la Mama yake na kufanya mwanamke huyo kukosa uhalali wa kugawana mali na hapo ndipo jina la Rais wa Wanaume lilipoanzia.