Familia

Raageshwari: Ajali ya ndege India yawaunganisha wanandoa

INDIA:NCHI ya India inaendelea kuomboleza maisha yaliyopotea katika ajali ya ndege ya Ahmedabad. Kuanzia kwa Shah Rukh Khan hadi Amitabh Bachchan, mastaa wa Bollywood wametoa masikitiko na salamu zao za rambirambi kwa wafiwa wote na taifa lao kwa ujumla, walakini, mwimbaji na muigizaji Raageshwari Loomba ameonesha utofauti aliposema ajali hiyo imesaidia kuwaunganisha wanandoa waliokuwa katika mgogoro wa muda mrefu.

Raageshwari aliingia kwenye Instagram na kushiriki video inayoangazia matokeo ya mkasa wa ajali ya ndege ya Ahmedabad. Amesema, “Je, unajua, baada ya ajali hiyo ya ndege yenye kuhuzunisha, watu walianza kuita familia zao? Najua wanandoa wawili walioamua kuachana na talaka zao. Familia ghafla ziliruhusu ubinafsi wao utulie, mabishano yao yatatuliwe. Ni nini kilibadilika? Wanasaikolojia wanasema sikuzote inachukua msiba kwetu sisi wanadamu kutambua mahali ambapo baraka zetu ziko, na hiyo ndiyo sababu maisha lazima yawe tofauti.”

Muigizaji huyo anasema jambo hilo ni la nadra sana kutokea kwa wanandoa kurudiana kwa sababu ya ajali lakini kwao kuna maana kubwa mno na namna ajali hiyo ilivyowakumbusha jambo ndiyo maana wamerudiana na kusahau changamoto zao zote.

“Wote tunahuzunika lakini nimeshuhudia familia hiyo licha ya kuhuzunika lakini huzuni hiyo imewafanya waitane kwa majina na kurudiana kama mke na mume sijui sababu hasa kwa nini imekuwa hivyo lakini kurudiana kwao ni furaha ingawa imesababishwa na jambo la majonzi” ameeleza muigizaji huyo wa India.

Ndege ya Shirika la ndege India, Boeing 787 iliyokuwa ikielekea London ilianguka alhamisi muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad, magharibi mwa India.

Katika ajali hiyo abiria mmoja mwanaume raia wa Uingereza ndiye mtu pekee aliyenusurika katika ajali hiyo na abiria wengine wote pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo wamefariki dunia ikiwa ni pamoja na raia 169 wa India na raia 52 wa Uingereza. Zaidi ya miili 200 ilipatikana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button