Kwingineko
PSG katika mtihani dhidi ya Bayern UCL

LIGI ya Mabingwa barani Ulaya(UCL) inarejea leo kwa michezo miwili hatua ya 16 bora huku kivutio kikiwa mchezo kati ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich kwenye uwanja wa Princes jijini Paris, Ufaransa.
Kwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana hatua ya robo fainali Aprili 13, 2021 Bayern Munich iliitoa PSG kwa sheria ya goli la ugenini.
Katika mchezo mwingine Tottenham Hotspur ni mgeni wa AC Milan kwenye uwanja wa San Siro jijini Milan, Italia.