Prince William anafikiria kurudi kwenye ngumi

WALES: BAADA ya mtoto mkubwa wa mfalme wa Uingereza, Charles III, Prince William kukabidhiwa glovu za mchezo wa ngumi na kocha Charlie Beatt wa kituo cha kubadilisha tabia za vijana wa mitaani ametamani kurudi katika mchezo wa ngumi licha ya kuona uwepo wa ugumu wa kazi hiyo.
Mwanamfalme huyo wa Uingereza, William alifanya mazoezi ya ngumi katika kituo hicho huku akielezea utayari wa aliokuwa akifanyanao mazoezi kituoni hapo: “Nyinyi mnaonekana tayari ni wataalamu! Mimi ninatoka jasho. Ninaweza kurudi kwenye ngumi! Imekuwa muda, muda mrefu kweli, lakini ni kazi ngumu sana.”
Mwanamfalme William ameeleza hayo wakati alipofanya ziara akiadhimisha miaka 20 kama mlezi wa kituo cha Centrepoint, ambapo ameshuhudia vijana wengi waliopo kituoni hapo wakibadilisha maisha yao.
Pia amecheza mpira wa meza na mmoja wa vijana kituoni hapo huku akisimuliwa namna kijana huyo alivyokosa makazi alipokuwa na umri wa miaka 17 lakini kwa usaidizi kutoka kituo hicho, alifanikiwa kupata nafasi katika Shule ya Uchuni katika jiji la London.
“Nilipowasiliana na Centrepoint, walinisaidia sana kila kitu kilichokuwa kikiendelea na hali yangu kilienda vizuri hadi nikaweza kwenda chuo kikuu, hali hiyo ni mabadiliko makubwa kwangu, bila wao sijui ningekuwa wapi?
Baada ya mchezo huo William alikubali ‘droo ya heshima’ ya 2-2 na kijana huyo kabla ya kuzungumza na mtendaji mkuu wa Centrepoint Seyi Obakin, ambaye alisisitiza umuhimu wa kuwapata vijana wa mtaani kwa ajili ya kuwafikisha katika kituo hicho kabla hawajaharibikiwa zaidi.
William ana miaka miwili katika mpango wake wa miaka mitano wa kukomesha ukosefu wa makazi kwa vijana wa mtaani yeye na mke wake




