Masumbwi

Maendeleo Benki Marathon kufanyika September 2

IMEELEZWA mashindano ya Marathon ya Maendeleo Benki yenye lengo la kusaidia vifaa vya afya kwa watoto wenye tatizo la usonji yatafanyika Septema 2 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Dk Ibrahim Mwangalaba amesema hatua hiyo imefuatiwa na benki kupata faida ya Sh bilion 144 na kufikisha wateja 600.

“Milion 200 zitatumika kununua vifaa vya watoto njiti na matembezi hayo yataanzia katika makao makuu ya benki hiyo hadi viwanja vya farasi jijini Dar es salaam lengo kukusanya Shilingi milion 200 kwa ajili ya watoto wenye usonji.”amesema Mwangalaba.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesemakuwa benki hiuyo kwa kuwa mdau mkubwa katika ukuajiwa sekta ya ajira nchini.

Amesema katika kipindi 2022/2023 imeweza kuwa na watumishi 114 huku tangia ianzishwe benki hiyo awali ilikuwa na watumishi 14 tu.

Related Articles

Back to top button