Mastaa

Pluto ajipa mapumziko baada ya kuachana na Felicity

NAIROBI: MTENGENEZA mahudhui mtandaoni, Thee Pluto, amethibitisha kuwa kwa sasa yuko single kufuatia kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Felicity Shiru.

Akizungumza katika mahojiano na Quick Fire, Pluto amesema kwa sasa ameamua kupumzika kutoka kwenye mahusiano.

“Niliachana na mahusiano miezi mitano iliyopita, hivyo niko kwenye mapumziko kwa sasa,” amesema.

Pluto pia alieleza kuwa alisoma Uchumi, ingawa awali alipelekwa kwenye Sayansi ya Uhalisia, na kazi yake ya kwanza ilikuwa Meneja Upataji wa Vipaji akilipwa Ksh 15,000.

Mtayarishaji huyo wa maudhui alithibitisha kuwa wameachana na Felicity mwaka 2024 baada ya Felicity kuondoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja kama mke na mume.

“Ni kweli tumeachana, lakini siwezi kufichua kila kitu kwenye mitandao ya kijamii. Tumeachana kwa amani. Tuna mtoto mmoja, hivyo ni muhimu kupeana heshima,” amesema Pluto baada ya miaka mitatu ya mahusiano yao.

“Tumeamua kujitenga na kukatisha uhusiano wetu wa miaka mitatu. Asante kwa familia, marafiki, na mashabiki. Tutaendelea kuwa wazazi wenza kwa amani na kuhakikisha binti yetu hapati athari kutokana na kutengana kwetu,” ameongeza.

Kwa upande wake, Felicity Shiru muda mfupi baada ya kutengana kwao, alishiriki vlog ikimuonyesha akihama kutoka kwenye nyumba yao ya zamani huku akiandika neno ‘MOVING OUT’.

“Nitakuwa nikiwinda nyumba, na kuna aina maalum ya nyumba ninayotafuta. Ninatumai, Mungu akipenda, nitapata ninachotaka,” amesema.

Alisema anahitaji nyumba ya vyumba viwili au vitatu kwa ajili yake, binti yake, dada wa kazi, na wageni wanaoweza kumtembelea.

“Sina hakika ni eneo gani nataka kuishi, lakini sitajiwekea kikomo. Hata hivyo, sitaki kukaa kando ya Barabara ya Thika. Watu wa Thika Road, sitaki kukaa huko. Nina sababu zangu, si kwamba Thika Road ni mahali pabaya,” amesema Felicity.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button