Onya kwa Mbappe, tetesi za usajili

REAL Madrid imemonya Kylian Mbappe kwamba itafuta kabisa nia yake ya kumsajili iwapo atasaini tena nyongeza ya mkataba Paris Saint-Germain.(El Chiringuito)
Wakala wa mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku ametoa ofa kwa Real madrid kumsajili mbelgiji huyo wakati mabingwa hao wa Ufaransa wakijiandaa kumkosa tena Mbappe.(El Debate)
Yametia Barcelona, Ansu Fati ameamua kuondoka Camp Nou na amechochea nia ya kumsajili kutoka vilabu vya Arsenal, Manchester United na Tottenham Hotspur. (AS
Joao Felix anayewaniwa na Barcelona anataka kuvunja mkataba wake na Atletico Madrid ingawa miaka minne imebaki kwenye mkataba huo. (La Sexta)
Liverpool imeimarisha mpango wa kumsajili kiungo wa Crystal Palace, Cheick Doucoure. (Independent)
Mchezaji mwingine katika rada ya Liverpool ni winga wa PSV Eindhoven, Johan Bakayoko na mazungumzo yamefanyika na wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuhusu uwezekano wa dili hilo.(Eindhovens Dagblad)
Chelsea na PSG zote zimefufua nia ya kumsajili kiungo wa Barcelona, Pablo Martín Páez Gavira maarufu Gavi.(SPORT)
Bayern Munich imefuta mpango wa kusaka golikipa mpya wa kikosi cha kwanza na inajiandaa kiweka imani kwa Sven Ulreich ingawa kipa mpya wa kusaidia anaweza kusajiliwa. (Bild)
Manchester United inafikiria kupata huduma ya kiungo wa Bayern, Ryan Gravenberch, nyota wa zamani wa Ajax chini ya Erik ten Hag. (Alfredo Pedulla)
Baada ya West Ham United kukataa ofa ya pauni milioni 70 ya Manchester City, wagonga nyundo hao wamepandisha dau la kumnunua kiungo wake, mbrazil Lucas Paqueta kuwa pauni milioni 85. (Telegraph)
Manchester United inajiandaa kumruhusu beki wa kati Eric Bailly kuondoka kwa uhamisho huru majira haya ya joto na ina matumaini Fulham kufuatilia nia yake ya awali. (RMC Sport)
Bernado Silva anajiandaa kusaini mkataba mpya Manchester City utakaojumuisha kipengele cha kuachiwa cha pauni milioni 43 katika majira ya joto 2024.(El Chiringuito)