Filamu

Omotola: Nilikataa mikataba mikubwa ya fedha ili kujilinda

NIGERIA: Muigizaji mkongwe wa Nollywood, Omotola Jalade amesema angekuwa bilionea kama angekubali baadhi ya mikataba yenye faida kubwa iliyowahi kutolewa kwake katika maisha yake ya sanaa ya uigizaji.

Akizungumza katika kipindi cha The Afropolitan Show, Omotola alisema alikataa ofa kadhaa za kifedha kwa sababu zilikuwa zinakinzana na maadili na misimamo yake binafsi.

Alieleza kuwa ingawa ofa hizo ziliahidi kumletea utajiri mkubwa, aliamua kuziacha kwa sababu zilikwenda kinyume na imani yake.

Omotola amesema uamuzi alioufanya umempa utoshelevu wa maisha ambayo hayawezi kupimwa kwa kiasi chochote cha fedha.

Related Articles

Back to top button