Ligi KuuNyumbani

Nikiri mambo magumu kwetu-Ahmed

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema sare timu yake iliyopata dhidi ya Kagera Sugar Disemba 21 imezidisha ugumu katika mapambano ya kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na SpotiLeo Ahmed amesema kuwa nyuma kwa tofauti ya pointi sita siyo jambo dogo hasa unaposhindana na timu ambayo kila siku inapata ushindi.

“Nikiri mambo yanazidi kuwa magumu kwetu sioni wenzetu kama wanaweza kudondosha pointi kirahisi hivi inaumiza sana lakini ndio mchezo wa soka unavyokua,” amesema Ahmed.

Amesema Simba itaendelea kupambana katika mechi zijazo na kuhakikisha inapata ushindi mpaka mechi ya mwisho ya ligi.

Sare hiyo imeiweka Simba nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 38 nyuma ya watani zao Yanga wenye pointi 44 huku kila timu ikiwa imecheza mechi 17.

Related Articles

Back to top button