Africa
Ni ‘La Revancha’ leo

KLABU ya Azam leo itashuka dimbani Dar es Salaam kuivaa Bahir Dar Kenema ya Ethiopia katika mchezo wa marudiano raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo ambao Azam imeupa kauli mbiu ‘La Revancha’ kwa maana ya kisasi utafanyika uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Agosti 20 kwenye Uwanja wa Abebe Bikila uliopo mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Azam ilipoteza kwa mabao 2-1.