
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inarejea leo baada ya mapumziko ya michezo ya timu ya taifa kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam na Mwanza.
Kivutio kikubwa ni mchezo kati ya Yanga na Azam kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 6 baada ya michezo miwili wakati Azam ipo nafasi ya 5 ikiwa pointi 4 baada ya idadi kama hiyo ya michezo.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu kati ya timu hizo, Yanga iliifunga Azam mabao 2-1 kwenye uwanja wa Azam Complex Aprili 6, 2022.
Katika mchezo wa pili Geita Gold itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Geita Gold ipo nafasi 13 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo miwili wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 16 bila pointi.