Kwingineko

Neymar:Situjitii kuichagua Barcelona juu ya Madrid

NEYMAR Jr amefunguka kuhusu kuondoka Barcelona na maisha yake PSG
Katika mahojiano maalumu na mchezaji wa zamani wa Brazil Romário. Katika mahojiano hayo Neymar alisema hana majuto yoyote kuhusu maamuzi aliyowahi kufanya katika maisha yake ya soka. Alieleza kuwa makosa aliyofanya yalichangia kumkuza na kumkomaza.
Alifichua kuwa hakuijutia kabisa hatua ya kujiunga na Barcelona badala ya Real Madrid, kwani alifuata moyo wake. Neymar amesema alitamani sana kucheza na Messi na kujiunga na klabu aliyokuwa akiipenda tangu enzi za Ronaldinho.
“Nilikuwa na siku ngumu sana. Kwa siku mbili au tatu sikufanya mazoezi kabisa, nilikuwa nina kazi ya kushughulikia hili. Watu wa Real Madrid walikuwa wakinipigia simu upande mmoja, na watu wa Barcelona upande mwingine. Marais wa klabu zote mbili walikuwa wakizungumza nami. Sikuweza kufikiri vizuri. Nilijiona nikicheza kwa klabu zote mbili… Lakini hatimaye moyo wangu uliongea kwa sauti kubwa zaidi. Niliamua kuchagua Barcelona.”
Kisha Neymar aliongeza kwa kusema”Sijutii uamuzi wangu wa kuchagua Barcelona badala ya Real Madrid. Nilifuata moyo wangu. Nilikuwa nataka sana kucheza na Messi! Barca ilikuwa timu niliyokuwa nikiipenda. Tangu enzi za Ronaldinho, daima nilikuwa nikisema: Nataka kucheza pale. Na ilitokea.”
Neymar alijiunga na Barcelona mwaka 2013 akitokea klabu ya Santos, alihudumu hadi mwaka 2017 akiwa ameichezea michezo 186,akifunga mabao 105 na kutoa pasi 76 za mabao.

Related Articles

Back to top button