Tetesi

Newcastle yamtupia macho Ferran Torres

TETESI za usajili zinaeleza kuwa klabu ya Newcastle United inavutiwa na fowadi wa Barcelona, Ferran Torres, mwenye umri wa miaka 23.(Fichajes – in Spanish)

Chelsea, Liverpool na Manchester City zinamfuatilia beki Mcanada wa Bayern Munich, Alphonso Davies mwenye umri wa miaka 23 lakini zinafikiri anataka kujiunga na Real Madrid. (90min)

Newcastle inapima uwezekano wa kumsajil beki mjerumani wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah mwenye umri wa miaka 27, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 20 Januari, 2024.(Sun)

Chelsea ipo tayari kushindana na Arsenal na Liverpool kumsajili kiungo mbrazil, Gabriel Moscardo mwenye umri wa miaka 18 ambaye anaweza kugharimu pauni milioni 26. (Standard)

Manchester United inafikiria kutuma ofa kumsajili mshambuliaji wa Lecce kutoka Montenegro, Nikola Krstovic mwenye umri wa miaka 23.(Calciomercato via TeamTalk)

Related Articles

Back to top button