Newcastle yakaribia kunasa saini ya Isak

KLABU ya Newcastle United inakaribia kuvunja rekodi yake ya ada ya uhamisho kwa kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad Alexander Isak kwa pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 163,868,256,000.
Agosti 24 mazungumzo zaidi yalifanyika baada ya Sociedad kuonesha wana nia kukubali muundo wa malipo ya uhamisho.
Mkurugnzi wa michezo wa Newcastle Dan Asworth alikuwa Hispania kukamilisha vipengele na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden ambaye ni kipaumbele cha kwanza cha klabu hiyo lakini amekuwa akifikiriwa kuwa ni uhamisho mgumu.
Ada hiyo inazidi ile ya pauni milioni 40 sawa na shilingi bilioni 109,245,504,000 iliyolipwa kwa timu ya Hoffenheim mwaka 2019 kwa ajili Joelinton Cássio Apolinário de Lira na Lyon kwa ajili ya Bruno Guimaraes Januari 2022.
Newcastle imekuwa ikisaka fowadi mpya kutokana na utimamu wa mwili wa Callum Wilson kutokuwa sawa.
Isaka amefunga mabao 44 katika michezo 132 aliyocheza Sociedad na amekuwa mmoja wa wachezaji wanaosaidia klabu hiyo.