Ligi Kuu

Mwalimu afungiwa michezo mitatu

DAR ES SALAAM : MCHEZAJI wa Simba, Seleman Mwalimu amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa Dodoma Jiji Andy Bikoko  wakati mchezo wa Ligi Kuu uliokutanisha timu hizo.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti.

Wachezaji wengine waliofungiwa ni beki Abdi Banda wa Dodoma Jiji amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kufanya kitendo kisicho cha kiuanamichezo na kinachokinzana na maadili ya mchezo wa mpira wa miguu, kwa kujirusha kutoka kwenye machela, kitendo kilichotafsiriwa kama hila ya kupoteza muda.

Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji huyo alipokuwa amebebwa kutolewa nje kwa maelekezo ya mwamuzi baada ya kupata maumivu.

Katika hatua nyingine, Bikoko wa Dodoma Jiji, Muhsin Malima Makame na Mzamiru Yassin wa TRA United wametozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja kwa kosa la kuchelewa kwa makusudi kuingia uwanjani kwa kile kilichoonekana ni kukwepa kupeana mikono na waamuzi na wachezaji wa timu pinzani katika mchezo uliozikutanisha timu hizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button