
KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Patrick Odhiambo amesema changamoto kubwa iliyopo kwenye kikosi chake ni kujenga muunganiko.
Akizungumza na Spotileo, kocha huyo raia wa Kenya ameeleza kuwa pamoja na kuanza vibaya msimu lakini anapambana kuhakikisha anaondoa tatizo hilo.
“Sijafuraishwa na kiwango ambacho tumeonesha tangu msimu uamze lakini najua tatizo ni kukosekana kwa muunganiko mzuri wa timu yangu,” ameeleza Odhiambo.
Kocha huyo amesema kwa kushirikiana na wasaidizi wake wanaendelea kutoa maelekzo ili kuanza kupata matokeo mazuri na kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Tanzania Prisons ilianza Ligi Kuu kwa kipigo cha bao 1-0 Augosti 16 kutoka kwa Singida Big Stars, ikashinda mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji Agosti 20 kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 Septemba 9 dhidi ya Mbeya City.