Nyumbani

Moro Youth yatamba ukuzaji vipaji nchini

TAASISI ya Kukuza na Kulea Vipaji vya Soka kwa Vijana Morogoro (Moro Youth) imefanikiwa kuibua na kukuza vipaji wa soka kwa  mamia ya vijana  ambao miongoni mwao wamefanikiwa kucheza timu ya Taifa ya wakubwa na wengine timu ya Taifa ya vijana.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Madundo Mtambo alisema hayo ,wakati wa bonaza la mchezo wa soka kati ya timu ya Moro All Stars dhidi ya Moro Kids  kwa ajili ya  kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mkoani Morogoro.

Profesa Madundo ambaye aliwahi kuchezea  timu za soka ya Reli Kiboko cha Vigogo nyakati hiyo pamoja na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) , kwa  sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Uendelezaji Viwanda Tanzania (TIRDO).

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, alisema kuwa hadi sasa Taasisi hiyo ina vijana zaidi ya 200 katika  kituo hicho.

“ Miaka 25 ya Kituo hiki vijana wengi wamnepita kwetu walikuwa na miaka 10 kwa sasa wamefikisha zaidi ya miaka 25 na wanaumri mkubwa “ alisema Profesa Madundo

Profesa Madundo alisema Kituo hicho kimepata mafanikio makubwa ikiwa na kutoa zaidi ya vijana 17 waliopitia ambao walikuwa  kwenye timu ya Taifa ya wakubwa  na vijana 19 kwenye timu ya Taifa ya Vijana .

“ Bado tunavijana wengi ambao wapo kwenye timu za ligi kuu , ligi daraja la kwanza na ligi zingine za ngazi mbalimbali “ alisema Profesa Madundo

Profesa Madundo aliwashukuru wadau mbalimbali wa mpira wa miguu wa mkoa wa Morogoro , serikali ya mkoa huo na Meya wa Manispaa ya Morogoro kwa kuwa karibu na Kituo hicho kwa kuwaunga mkono.

Pia aliwashukuru baadhi ya wachezaji waliopitia kwenye Kituo kwa kutenga muda wao kwa kufika kuungana katika bonaza la  maadhimisho ya miaka 25  ya kituo hicho.

Naye mchezaji anayetokana na zao la Kituo hicho , Shomari Kapombe ambaye kwa sasa ni mchezaji nguli wa  timu ya Simba alisema, ni jambo la furaha  kujumuisha na wachezaji waliotokana na kituo hicho na kucheza  kwenye uwanja wa SabaSaba ambao uliwakuza chini ya walimu mbalimbali wa soka wa kituo hicho.

“ Ni jambo la furaha kukutana na wenzagu tunaotokana na kituo hiki na kumecheza mpira tena kwenye uwanja huu ambao ndiyo chimbuko letu sote , tumeonesha  kipaji chetu cha  soka nikiwemo mimi  mwenyewe na pia kukutana na viongozi wetu “ alisema Kapombe

Alisema wachezaji wengi anaotamba katika timu mbalimbali nchini  ni zao la kituo hicho , hivyo aliamua kuja kuwatia moyo waliopo kwa sasa kuwa wasikate tamaa ila  waongeze bidiii.

“ Ninawambia vijana kuwa  neno mafanikio ni neno dogo lakini linauzito mkubwa , na mafanikio kuyapata inaabidi kupambana , upambanie hilo neno mafanikio  kwa kuweka  malengo yanayofikiwa   bila kusahu nidhamu ndani ya mchezo nan je ya mchezo” alisema Kapombe

Taasisi hiyo imezalisha wachezaji wengi wanawika katika medani ya soka nchini wakiwemo  Shomari Kapombe, Kibwana Shomari, Mzamiru Yassin , Shizya Kichuya , Dickson Job , Zawadi Mauya , Kassian Ponera, Jaffary Kibaya  na  Edward  Christopher ambao wengi walishiriki katika bonaza hilo ambalo liliambatana na utoaji wa tuzo kwao.

Related Articles

Back to top button