
KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema pamoja na mwenendo usioridhisha wa timu yake Ligi Kuu Tanzania Bara bado anaamini itafanya vizuri katika michezo iliyobaki ili kujiweka katika mazingira salama.
Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema matokeo kama hayo yanaweza kuitokea klabu yoyote duniani cha msingi sasa ni kuhakikisha mapungufu yanarekebishwa ili kupata pointi tatu kila mchezo.
“Ligi ni ngumu na ushindani ni mkali kitu cha msingi tunapaswa kuichukia hali hii na kubadilisha matokeo ndani ya uwanja. Hiki ni kipindi cha mpito naamini kitapita,” amesema Mkwasa.
Mkwasa, kiungo wa zamani wa Yanga, amesema kutetereka kwa kiwango cha Ruvu kunatokana na baadhi ya wachezaji muhimu kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi.
Ruvu shooting inashika nfasi ya 13 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 11 ikiwa imeshinda mitatu, sare mbili na kupoteza michezo sita.