Mitindo

Miss Tanzania 2023 Tracy kumchagua Miss Burundi

DAR ES SALAAM: MISS Tanzania 2023, Tracy Nabukeera, anatarajiwa kuwa mgeni maalum katika fainali za kumchagua mrembo wa Burundi zitakazofanyika Ijumaa ya Julai 25, mwaka huu nchini Burundi.

Nabukeera amekabidhiwa rasmi bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo nchini humo.

Akizungumza baada ya kupokea bendera hiyo Tracy alionesha furaha yake kubwa kwa nafasi hiyo adhimu ya kulitumikia Taifa kupitia tasnia ya urembo.

“Ni heshima kila wakati kubeba bendera popote niendapo. Nimejaa furaha na msisimko kushuhudia na kusherehekea uzuri, utamaduni na vipaji vya dada zetu wa Burundi. Ninamshukuru Mungu kwa safari hii na kwa fursa ya kuunganishwa, kuhamasisha na kujenga madaraja ya maelewano zaidi ya mipaka,”alisema.

Tracy tayari amekabidhiwa bendera ya Taifa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ikiwa ni ishara ya kupeperusha heshima ya Tanzania katika jukwaa hilo la kimataifa la urembo litakalohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Burundi na Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button