Serie A

Milan yamla kichwa Conceicaio, Allegri ndani

MILAN: MABINGWA wa zamani wa Serie A, AC Milan wamemtimua Sergio Conceicao kama ilivyotarajiwa jana Alhamisi kufuatia msimu mbaya ambao kikosi hicho kilishindwa kufuzu kwa michuano ya ulaya msimu ujao, huku mabingwa hao mara saba wa Ulaya wakimtangaza Massimiliano Allegri kuwa kocha mpya.

Milan iliyomaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A, pointi 19 nyuma ya bingwa wa Italia, Napoli. Wamemshukuru Conceicao kwa kazi yake iliyotuka klabuni hapo na kumtakia heri yeye na wasaidizi wake huko waendako.

“Klabu ingependa kumshukuru Sergio na wasaidizi wake kwa kujitolea kwao, taaluma na kujitolea kwao na kazi ‘iliyotukuka’ wakati wanakiongoza kikosi chetu cha kwanza katika miezi michache iliyopita,” – taarifa hiyo ilieleza

Conceicao alirithi mikoba ya kuinoa Milan kutoka kwa Paulo Fonseca aliyetimuliwa mwezi Desemba na kumpa mkataba wa miezi 18 na mara moja akaiongoza Milan kutwaa ubingwa wa Kombe la Super Cup la Italia nchini Saudi Arabia katika mechi zake za kwanza kama kocha.

Ndoto mbaya zilianza wakati Milan ilipotolewa na Feyenoord katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Februari kisha ikafungwa na Bologna katika fainali ya Kombe la Italia mwezi huu. Wakati wapinzani wao wa jiji, Inter Milan watacheza na Paris Saint-Germain katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi.

Massimiliano Allegri sasa ndiye kocha atakayetekalia benchi la ufundi la Milan na kuiongoza klabu msimu ujao huku akiwa na kumbukumbu ya kuipa AC Milan hiyo taji la Serie A mwaka 2011 ukiwa ni msimu wake wa kwanza. Akiwaacha mahasimu wao Inter kwa pointi 6 kabla na kumaliza ukame wa miaka 7 wa taji hilo kabla ya kutimuliwa mwaka 2014 akiiacha AC milan katika nafasi ya 11 kweye msimamo wa Serie A.

Kazi mbili za mwisho za Allegri zilikuwa Juventus. Alitimuliwa na Bianconeri (Juventus) mwaka mmoja uliopita kwa kutoa kauli mbaya kwa waamuzi wakati wa fainali ya Kombe la Italia. Kocha huyo alishinda taji lake la kwanza na Milan Mwaka 2011 kisha kushinda mataji Matano mfululizo kuanzia 2015 hadi 2019.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button