Muziki
Mbosso awaandaa mashabiki wake

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Mbwana Kilungi ‘Mbosso’, ameweka wazi kwa mashabiki wake kuwa kwa sasa wanapaswa kutarajia kazi bora zaidi kutoka kwake kila wanaposikia jina lake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliandika ujumbe unaoonesha dhamira yake ya kuendelea kutoa muziki wenye ubora na maudhui mazuri kwa mashabiki wake.
Katika ujumbe huo, Mbosso ameandika:“Unaposikia ‘Mbosso Khan Tenaa’ hutarajii kitu kingine zaidi ya muziki safi na chanya.”
Maneno hayo yamepokelewa vyema na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakionesha imani yao kuwa msanii huyo.




