Nyumbani

Mbegu, Lyanga wapewa mtihani mzito Mashujaa

DAR ES SALAAM: NYOTA wawili waliosajili dirisha dogo na timu ya Mashujaa FC, Daniel Lyanga na Yahaya Mbegu, wanakibarua kigumu cha kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Nyota hao wamesajiliwa kuongeza nguvu safu ya ulinzi katika michezo 16 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara,wameruhusu mabao 14 sawa na idadi ya mabao waliofunga

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Abdallah, ‘Bares’, amesema wanaimani kubwa maingizo mapya ya usajili wa dirisha dogo kwani utasaidia kusahihisha makosa yaliyofanyika kwa nusu msimu wa wa ligi hiyo.

“Ni kweli hatukuwa vizuri kipindi cha mzunguko wa kwanza kwa sababu idadi ya mabao tuliyofunga ni sawa tuliyofungwa, tunaimani na wachezaji wapya waliosajiliwa dirisha dogo,” amesema.

Bares ameongeza kuwa safu ya ulinzi na ushambuliaji ilikuwa na mapungufu na wamefanyia kazi kwa kuondoa makosa kwa kufanya mazoezi na sasa wanacheza mechi za kirafiki kujiweka sawa kabla ya kurejea kwa ligi kuu.

“Tunaenda kwenye ushindani mkubwa tunatambua mzunguko wa pili, mgumu sana tunatakiwa kujipanga vizuri kipindi hiki cha maandalizi kabla hatujaenda Mbeya kucheza dhidi ya Tanzania Prisons,” amesema.

Kocha huyo amesema watakuwa na mechi nne za kirafki kufikia mipango yake na kujiridhisha na sehemu ya mafunzo anayowapa wachezaji katika nafasi ya ulinzi na ushambuliaji.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button