
KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa ametamba kikosi chake kuibuka na ushindi Septemba 29 dhidi ya Coastal Union.
Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Coastal Union ikiwa ni moja ya mechi mbili katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanznaia Bara.
Akizungumza na Spotileo, kocha huyo huyo amesema anawajua vizuri wapinzani wao na wamekuwa na rekodi ya kuwafunga kwahiyo pointi tatu ni lazima kesho.
“Tunawaheshimu Coastal Union lakini naamini utakuwa mchezo wenye faida kwetu kutokana na kucheza nyumbani tena tukiwa tumeimatoka zaidi baada ya mapumziko,” amesema Mkwasa.
Kocha huyo ameeleza kuwa anajua ugumu utakuwepo kwambali kutokana na wapinzani wao kubadili kocha lakini hilo siyo tatizo kubwa kwao.
Ruvu inashika nafasi ya saba kwenye msimamo ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili kati ya nne walizocheza.