Kwingineko

Mbadala wa VAR kuanza majaribio Australia

SYDNEY: SHIRIKISHO la Soka nchini Australia (Football Australia) limesema Ligi ya Championship ya Australia itafanya majaribio mfumo mpya wa usaidizi wa waamuzi wa FIFA wa Football Video Support (FVS), toleo dogo la mfumo wa Video Assistant Referee (VAR), wakati wa michezo ya mtoano ndani ya wiki chache zijazo.

FVS imetengenezwa na shirikisho la soka duniani kukidhi mahitaji ya nchi na ligi ambazo hazina rasilimali za kifedha za kuendesha VAR, ambayo sasa imeenea katika mashindano ya kimataifa na klabu kubwa.

Badala ya kuwa na afisa wa VAR kando ya uwanja akitazama video ya mchezo na kuwasiliana na referee, FVS itatumika pale tu ambapo makocha wataomba mapitio ya matukio katika idadi ndogo ya matukio wakati wa mchezo.

Makocha wanaweza kuomba mapitio tu kwa kesi za mabao, penalti, kadi nyekundu za moja kwa moja na katika hali ambapo wanaona mwamuzi amemuadhibu mchezaji asiye sahihi kwa kadi nyekundu.

Kisha referee atatazama video kwenye skrini iliyoko kando ya uwanja na kuthibitisha au kubatilisha uamuzi wake. FIFA inatarajia idadi ndogo ya engo za kamera inaweza kusababisha baadhi ya uamuzi kubakia vilevile kutokana na ushahidi usiokamilika.

FIFA tayari imejaribu mfumo huu katika mashindano ya kimataifa ya vijana ambapo makocha waliruhusiwa malalamiko mawili kwa kila mchezo, na mapitio yenye mafanikio kuendelea.

A-League ya Australia ilikuwa ligi ya kwanza ya ndani duniani kuanza kutumia VAR mnamo mwaka 2017.

Championship ya Australia ilianzishwa mwaka huu kama ligi Daraja la pili kitaifa na imepata mafanikio makubwa na mvuto kwa mashabiki.

“Kuzindua Football Video Support kunalingana na aina ya shirikisho tunalotaka kuwa, shirikisho ambalo linakumbatia uvumbuzi, linasukuma mipaka na daima linatafuta njia mpya za kuinua mashindano yetu,” amesema mkurugenzi mtendaji wa Football Australia, Heather Garriock.

“Tutashirikiana kwa karibu na FIFA wakati wote wa majaribio kuhakikisha mfumo huu unaimarisha viwango vya mchezo lakini pia kuangalia jinsi FVS inaweza kuanzishwa katika mashindano mengine nchini Australia.”

Related Articles

Back to top button