Wasifu

Mayele mchezaji bora DR Congo

MSHAMBULIAJI wa Yanga Fiston Mayele ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa mwaka 2022.

Tuzo hizo zimetolewa na mtandao, Leopard Foot wa DR Congo, na Mayele kufanikiwa kuwabwaga wenzake kwa ushindi wa asilimia 81.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Yanga Mayele amesema ni jambo kubwa kwake kama mchezaji kushinda tuzo hiyo.

“Nafurahi sana kushinda tuzo hii ya mchezaji bora wa mwaka wa DR Congo.Tuuanze mwaka 2023 kwa nguvu kubwa ya kuipambania timu yetu izidi kupata mafanikio,” amesema Mayele

Amewashukuru mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kumpigia kura.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button