Habari Mpya
Mayay Kaimu Mkurugenzi Michezo

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imemteua Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, John Mapepele imesema Mayay anachukua nafasi ya Yusuph Omary Singo aliyepangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huo unaanza leo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi huo ni katika kuimarisha utendaji Sekta ya Maendeleo ya Michezo na kufuatia maelekezo ya Waziri wa wizara hiyo Mohamed Mchengerwa.
Mayay alikuwa Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege.