Maumivu ya sikio yamsababishia Adele ukiziwi

LAS VEGAS: MKALI wa wimbo wa ‘Hello’ Adele Adkins alipokuwa katika onesho lake la Los Vergas ‘Weekend With Adele’ ameeleza namna alivyopatwa na maumivu katika masikio yake akidai kwamba hajawahi kupata maumivu kama hayo katika maisha yake yote.
Mwimbaji huyo mwenye miaka 36 mwenye mtoto wa kiume Angelo mwenye miaka 12, aliyezaa na mume wake wa zamani Simon Konecki mapumziko yake katika mji wa Sin City yanaelekea mwisho.
Adele amewaambia mashabiki zake kwamba alikumbwa na maambukizi yaliyokuwa yakimletea maumivu makali kuliko hata uchungu wa kujifungua.
Akizungumza jukwaani mbele ya mashabiki zake katika onesho lake la Las Vegas ‘Weekend With Adele’ alifafanua: “Nina changamoto kwenye sikio ambayo inanipa maumivu makali.
“Sikuwahi kuwa nayo kabla. Ni maumivu makali sana ambayo hayajawahi kunikumba. Ni makali zaidi ya uchungu wa kujifungua.”
Adele kwa sasa anakaribia kumaliza mapumziko yake katika makazi yake huko Sin City huku akidai kwamba “hatosahau bakteria adimu kweye maji waliomsumbua katika masikio yake na ikwawa ngumu kwake kuyatibu.
Mwimbaji huyo amesema alitumia dawa za kuua vidudu na kuondoa sumu ili kutibu maradhi hayo lakini amedai awali aliandikiwa dawa zisizo sahihi kwa kwani zilimsaidia kwa siku chache lakini maumivu yalizidi kiasi kwamba alitaka kukata sikio lake kutokana na maumivu hayo.
Alisema: “Nilikuwa nikitumia dawa zisizo sahihi kwa siku chache, kisha walinipa dawa nyngine ambayo ilifanya kazi lakini nilitaka kukata sikio langu kwa maumivu.
“Kwa sasa sina uchungu tena, lakini mimi ni kiziwi kidogo katika sikio langu la kushoto!”
Wakati huo huo, mwimbaji huyo wa ‘Someone Like You’ – ambaye sasa amechumbiwa na wakala wa michezo Rich Paul ni mpenzi wa paka na alifichua kwamba ameunda chumba maalum katika jumba lake la kifahari ili aweze kuokoa moggies wengi siku moja.
Alisema: “Nitakuwa mama wa paka wa dharura mara tu nitakapohamia katika nyumba yangu mpya. Nimeunda chumba ambacho mchumba wangu hakijui nitajengea kreti nyingi ukutanihatoweza kujua hilo … lakini kwa sasa anaweza kujua kwa sababu nimeliweka wazi jukwaani.”