Ligi KuuNyumbani

Mashujaa yashusha chuma cha Burundi

WABABE wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Mashujaa imeendelea kuimarisha kikosi chake safari hii ikishusha chuma kutoka Burundi, Kelvin George.

Mashujaa ambaye imepanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao tayari imewasajili Omary Kindamba, Maicon Masinda, Nassor kiziwa na Abdulnasir Asaa Mohamed (Gamal) huku ikimteua Abdallah Barres kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.

“Kelvin George, Tumeinasa saini yake kutoka kwenye klabu ya “Bumamuru FC ya nchini Burundi 🇧🇮. Sifa ya Kelvin George, anajua ni wakati gani wa kukokota mpira au kutoa pasi, anajua kufunga, anajua kuchezesha timu, ana uwezo wa kuficha mpira,”imesema taarifa ya Mashujaa.

Klabu ya Bumamuru ndio mabingwa wa ligi Kuu ya Burundi msimu uliomalizika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button