
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili Dar es Salaam na Kigoma.
Bingwa mtetezi Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 65 baada ya michezo 25, itaikaribisha Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 30 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Mashujaa inayoshika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 25 ambayo ipo katika hatari ya kushuka daraja itaikabili KMC iliyopo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 33 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.