Ligi Kuu

Mashabiki waikamua Pamba Jiji Mil. 2

DAR ES SALAAM: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara TPLB imeitoza Klabu ya Pamba Jiji FC ya Jijini Mwanza faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea (Pitch) ya Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza mara baada ya mchezo wao dhidi ya Azam FC kumalizika.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo imeeleza kuwa Kitendo cha mashabiki hao kuingia kiwanjani kilisababisha kuvunjika kwa mahojiano ya makocha yaliyokuwa yakifanywa na mdhamini mwenye haki ya matangazo ya runinga kituo cha televisheni cha Azam TV.

Aidha Bodi ya ligi kuu imezielekeza klabu zote, wasimamizi wa vituo na maofisa wengine wa michezo ya ligi wakiwemo maofisa usalama, kuhakikisha matukio ya aina hii hayatokei tena viwanjani kwasababu yanahatarisha usalama na kuchafua hadhi ya ligi.

Taarifa imeenda mbali na kusema kuwa uwanja wowote ambao litatokea tukio la mashabiki kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch) kabla, wakati au baada ya mchezo wa Ligi, basi uwanja huu utafungiwa kutumika kwa michezo ya ligi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button