Kwingineko

Marcus Thuram amwaga wino Inter

MIAMBA ya soka Italia, Inter Milan imemsajili winga wa Ufaransa Marcus Thuram kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake katika klabu ya Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, Borussia Monchengladbach kufikia tamati.

Marcus mwenye umri wa miaka 25 ni mtoto wa beki wa zamani wa Barcelona na Juventus Lilian Thuram ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ufaransa mwaka 1998.

Marcus amecheza mechi 134 akiwa Monchengladbach akifunga magoli 44 katika misimu minne.

Alihamia Bundesliga mwaka 2019 akitokea klabu ya Guingamp iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Aprili mwaka huu Monchengladbach ilithibitisha kwamba winga huyo hata saini mkataba mpya, hivyo kuhusishwa na kuhitajika vilabu kadhaa Ulaya.

Related Articles

Back to top button