Mama wa Mariah Carey, dada yake wafariki siku moja
NEW YORK, Marekani: MAMA wa mwimbaji maarufu wa muziki wa R&B, Mariah Carey, Patricia mwenye miaka 87 na dada yake Alison mwenye miaka 63 walifariki dunia siku moja.
Mwanamuziki huyo mwenye miaka 55 alitangaza tukio hilo la majonzi akisema: “Moyo wangu umevunjika kwamba nimempoteza mama yangu wikiendi iliyopita. Cha kusikitisha ni kwamba, katika hali mbaya, dada yangu alipoteza maisha siku hiyo hiyo. Ninahisi kubarikiwa kwamba niliweza kutumia wiki iliyopita na mama yangu kabla hajafariki.
“Ninathamini upendo wa kila mtu na msaada na heshima kwa faragha yangu wakati huu mgumu.”
Mwimbaji huyo wa ‘Always Be My Baby’ hakuweka wazi zaidi kuhusu matukio yaliyosababisha vifo vya wapendwa wake hao zaidi ya kutangaza masikitiko hayo.
Mama wa mwimbaji huyo Patricia alitalikiana na Alfred Roy Carey mwaka wa 1973 ambaye naye ni marehemu, alikuwa mwimbaji na kocha wa sauti kabla ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Akiandika katika mada yake ya 2020 ‘Maana ya Mariah Carey’, alisema: “Kama nyanja nyingi za maisha yangu, safari yangu na mama yangu imekuwa imejaa utata na ukweli unaoshindana. Haijawahi kunyooka imekuwa na mambo mengi yakiwemo kiburi, maumivu, aibu, wivu na tamaa.