Masumbwi

Mafia Boxing yagawa gesi kwa wajasiriamali

DAR ES SALAAM:KAMPUNI ya Mafia Boxing Promotion imegawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Magomeni Sokoni ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuondokana na matumizi ya nishati ya mkaa.

Mama lishe hao, zaidi ya 30, wamepatiwa majiko hayo wakati wa kuwatambulisha mabondia 14 watakaopanda ulingoni leo kwenye Knockout ya Mama.

Akizungumza baada ya kugawa majiko hayo, Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba, amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanaunga mkono harakati za Rais Samia za kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa Watanzania.

“Rais wetu, Dk. Samia, amekuwa akihamasisha Watanzania kuachana na matumizi ya nishati chafu kama mkaa na kuni. Nasi tukaona hatuna budi kuunga mkono jitihada hizo kwa kugawa majiko kwa mama lishe wenye mahitaji katika soko hili la Magomeni,” amesema Zayumba.

Baadhi ya mama lishe waliopata majiko hayo ni Zubeda Idd, Anna Joseph, Halima Tumbo, Shufaa Abras, Rehema Singa, Zarau Omari, Asha Bindu, Theresia Vincent na wengineo, ambao waliishukuru Mafia Boxing Promotion kwa msaada huo, wakisema utawasaidia kupika kwa haraka na kwa muda mfupi.

Zayumba pia alizindua makala maalum na kuwaonesha wananchi namna ambavyo Rais Samia amekuwa msaada kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kuinua michezo bila ubaguzi, huku akimshukuru kwa kuwa pamoja nao.

Related Articles

Back to top button