Ijue Sheria namba 17 ya soka
Sheria namba 17 Pigo la kona.
–
Katika sheria 17 za soka sheria ya mwisho ya 17 ni kona. Fifa wameeleza nini maana ya kona.
–
Fifa wanasema: Kona ni njia ya kuanzisha upya mchezo.
–
Fifa wanasema ili mpira upigwe kona lazima uwe umevuka wote kwenye mstari wa goli yaani ‘Goal Line’ na sharti mpira uguswe na mchezaji wa timu inayoshambuliwa iwe chini au angani.
–
Fifa wanasema: Bao linaweza kufungwa moja kwa moja na aliyepiga kona hiyo ila kwa sharti la timu inayoshambuliwa tu.
–
Sheria za kupiga kona
– Fifa wanasema kwanza mpira uwekwe ndani ya upinde wa kona karibu na kibendera cha kona ‘ flag post’ au usitoke ndani ya upinde huo.
– Flag post haipaswi kugosezwa kwa namna yoyote, na wapinzani lazima wabaki angalau mita 9.15 ( yards 10 ) kutoka eneo la mpira.
–
Mpira ukiwa katika mchezo
✍🏿 Mpira lazima upigwe na mchezaji wa timu inayoshambulia
✍🏿 Mpira utakuwa katika mchezo pindi utapopigwa na kuanza kuchezwa.
✍🏿 Mpigaji hapaswi kuucheza mpira mpaka utapoguswa na mchezaji mwingine.
–
Ukiukwaji wa sheria hizo nini kinatokea?
#Mpira wa kona uliopigwa na mchezani mwingine isipokuwa golikipa ikiwa baada ya mpira kuchezwa mpigaji akagusa mpira isipokuwa kwa mikono yake kabla haujaguswa na mchezaji mwingine!
1. Pigo la adhabu lisilo la moja kwa moja (indirect free kick) litatolewa kwa timu pinzania kutoka eneo tukio limefanyika.
#Ikiwa baada ya mpira kuchezwa, mpigaji ataingilia mpira kwa makusudi kabla ya mchezaji mwingine kuugusa
1. Pigo la moja kwa moja litaamuliwa kwa timu pinzani kutoka eneo la tukio.
2. Penalti itatolewa ikiwa mchezaji huyo atafanya hivyo katika eneo lake la penalti.
–
#Mkwaju wa kona uliopigwa na kipa.
–
Ikiwa, baada ya mpira kuchezwa, kipa atagusa mpira tena (isipokuwa kwa mikono yake) kabla haujagusa mchezaji mwingine:
* pigo la adhabu lisilo la moja kwa moja linatolewa kwa timu pinzani, itakayochukuliwa
mahali ambapo ukiukwaji ulifanyika.
–
Ikiwa, baada ya mpira kuchezwa, kipa ataushika mpira kwa makusudi kabla haujagusa mchezaji mwingine:
* pigo la adhabu la moja kwa moja litatolewa kwa timu pinzani iwapo ukiukaji huo utafanyika nje ya eneo la penalti la golikipa, pigo litachukuliwa mahali ambapo ukiukwaji ulifanyika.
* pigo lisilo la moja kwa moja litatolewa kwa timu pinzani ikiwa ukiukaji ulifanyika ndani ya eneo la penalti la golikipa, na kutolewa mahali ambapo ukiukwaji ulifanyika.