Tetesi

Liverpool yafikiria kumsajili Nunes

Liverpool wanafikiria kumsajili kiungo wa Wolverhampton Wanderers Matheus Nunes msimu ujao.

Kiungo wa Borussia Dortmund, mwingereza Jude Bellingham bado ni lengo kuu la Liverpool lakini Nunes anafikiriwa kuwa chaguo mbadala ikitiliwa maanani Chelsea, Manchester City na Real Madrid zinagombea saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham.

Liverpool pia itakuwa tayari kumsajili kiungo kwa mkopo mwezi huu iwapo mchezaji sahihi atapatikana.

Nunes mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Wolves Agosti, 2022 akitokea Sporting kwa uhamisho wa pauni milioni 38 sawa na shilingi bilioni 106.2.

Katika michezo 50 aliyocheza Sporting msimu uliopita Nunes alifunga mabao 4 na kuhusika katika mengine 5 akisaidia timu yake kutwaa Super cup na kombe la ligi nchini Ureno.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button