Tetesi

Liverpool yawasilisha ombi la awali kwa Alonso

TETESI za usajili zinasema Liverpool imewasilisha ombi la awali la kuzungumza na kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso wakati ikiendelea kusaka mbadala wa Jurgen Klopp anayeondoka. (Bild – in German)

Tottenham inapanga kusajili fowadi mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja majira yajayo ya kiangazi huku winga wa mreno wa Wolves, Pedro Neto, 23, na winga wa England anayekiwasha Crystal Palace, Eberechi Eze, 25, wakipewa kipaumbele kwa sasa.(Independent)

Manchester United itafanya maamuzi ya hatma ya fowadi wa England, 22, Mason Greenwood, ambaye sasa yupo kwa mkopo Getafe, ifikapo mwisho wa Mei, 2024. (Sun)

Arsenal, Manchester United na Chelsea zina nia kumsajili golikipa mjerumani Diant Ramaj, 22, anayecheza Ajax. (Bild)

Liverpool itaangalia uwezekano wa kumsajili winga mcameroon wa Brentford,’The Bees’, Bryan Mbeumo, 24, kwa bei ya mazungumzo iwapo The Bees itashuka daraja kucheza Championship. (Express)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button