Ligi Kuu Wanawake kuhitmishwa leo

Ligi kuu ya wanawake kwa msimu mwa mwaka 2022/2023 inafikia tamati hii leo kwa michezo ya mzunguko wa 18 kupigwa, ambapo vita kali ipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo mtifuano ukiwa ni wa farasi wawili.
Mabingwa watetezi Simba Queens wanachuana vikali na Jkt Queens ambao wamepishana kwa tofauti ya alama moja, Jkt Queens wanahitaji kupata ushindi dhidi ya Mkwawa Queens ili kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo, wakati Simba Queens wao wanahitaji kushinda dhidi ya Ceasiaa Queens na kumuombea Jkt Queens apoteze au kupata sare dhidi ya Mkwawa Queens.
Vita nyingine kwenye ligi hiyo ni ya kusalia kwenye ligi kwa msimu ujao ambapo Amani Queens na The Tigers Queens zote zina alama nane na mmoja ni lazima ashuke kuungana na Mkwawa Queens ambaye alishashuka daraja.