Lady Gaga, Mariah Carey, Taylor Swift watuzwa

LOS ANGELES: WANAMUZIKI wanawake watatu wa nguvu wameshinda tuzo za heshima kutoka kwa kamati ya Tuzo za iHeartRadio 2025 akiwemo Lady Gaga aliyepokea Tuzo ya ‘Innovator’, Mariah Carey akipokea Tuzo ya Icon, na Tamasha la ‘Eras Tour’ la Taylor Swift likishinda Tamasha Bora la Mwaka, limevunja rekodi mbalimbali na limemfanya awe mwanamuziki mwanamke aneyeongoza kwa mkwanja mrefu duniani.
Kamati ya Tuzo za Muziki za iHeartRadio, imetoa tuzo zake kwa wasanii mbalimbali kulingana na mafanikio waliyopata katika kazi zao za muziki wakiwemo Lady Gaga na Mariah Carey.
Tuzo hizo zinazotambua vipaji vikubwa vya muziki kwa mwaka zinafanyika kila mwaka na mwaka huu zimefanyika katika Ukumbi wa michezo wa Dolby huko Los Angeles, zilipofanyika Tuzo za Academy wiki chache zilizopita.
Wasanii wengine walioshinda tuzo mbalimbali ni pamoja na Nelly aliyepokea Tuzo la iHeartRadio Landmark, akiadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya albamu yake ya kwanza, ‘Country Grammar’, Albamu Bora imeenda kwa Beyonce kupitia albamu yake ya ‘Cowboy.
Tuzo ya Msanii Bora wa mwaka ikienda kwa Gracie, Msanii Bora wa R&B wa mwaka imekwenda kwa SZA AKISHINDA kwa mwaka wa tatu mfululizo akiweka rekodi ya kushinda tuzo hiyo mfululizo na Tuzo ya msanii Bora wa mwaka wa hip-hop imekwenda kwa GloRilla.
Lady Gaga amesema: “Kushinda tuzo ya kuheshimu taaluma yangu yote nikiwa na umri wa miaka 38 ni jambo gumu kuliweka kichwani mwangu, “Kwa upande mmoja, ninahisi kama nimekuwa nikifanya hivi milele, kwa upande mwingine, ingawa ulimwengu unaweza kumchukulia mwanamke aliye katika miaka ya hivi karibuni ya 30 kama nyota wa pop.