Kovac alia na muda, joto Marekani

EAST RUTHERFORD, Meneja wa Borussia Dortmund, Niko Kovac amelalamikia muda wa kuanza kwa mechi huku akitaka za baadaye zitazamwe upya baada ya wachezaji wake kuhangaika tena na joto kali katika kichapo cha 3-2 kutoka kwa Real Madrid katika mchezo robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu uliopigwa saa 9 mchana.
Dortmund imewahi kucheza katika hali ya hewa ya joto inayozidi nyuzi joto 90 za Selsiasi sawa na nyuzi 32 za sentigredi mwezi uliopita katika mchezo wa hatua ya makundi uliopigwa mjini Cincinnati.
“Wanamichezo hawa wanalazimika kujitolea kwa kiwango cha juu katika hali hii ngumu lakini watafanyaje na ndo aina ya mashindano? Tutaona kwenye kombe la dunia la mwaka ujao lakini Tunapaswa kuzingatia afya za wachezaji.” amesema Kovac
“Hali hii ni ngumu sana kwa mtu yeyote, na wachezaji lazima wacheze michezo hii Lakini Sawa, haya ndiyo mashindano, tunahitaji kucheza. Ni maoni yangu kwamba muda wa kuanza kwa mchezo ungesogezwa mbele kidogo . Tulicheza Atlanta saa 3 usiku na mchezo ulikuwa mzuri” – aliongeza
“Kama mtazamaji, ungependa kuona soka la nguvu, kali, na la vuta nkuvute lakini kukiwa na joto kali ni vigumu kucheza aina hii ya soka.” alimaliza Kovac
Hali ya hewa ya joto kali nchini Marekani imeibua hali ya wasiwasi katika Kombe la Dunia la Klabu linaloendelea hivi sasa na wasiwasi zaidi kuhusu Kombe la Dunia la 2026 litakalohusisha timu za ambapo kwa mara timu 48 zitachuana.
Shirikisho la soka duniani FIFA, limeweka ‘cooling break’ kama moja ya hatua za kupunguza joto lakini makocha na wachezaji bado wamelalamika juu ya muda ambao mechi zinachezwa ikiwa ni mchana wa jua na joto kali. Huku jumuia ya wachezaji duniani FIFPRO ikisema inatafuta njia bora ya kumlinda mchezaji