Ligi Kuu

KMC: Yanga mazoea yatawaponza!

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa KMC FC, Abdihamid Moallin, amesema kikosi chake kipo tayari kuwakabili Yanga katika mchezo wa kesho, Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi.

Amesema anaiheshimu Yanga na hayupo tayari kufanya makosa ya msimu uliopita kwa kuwa anahitaji kufanya vizuri ili kuondoka na pointi muhimu mbele ya wenyeji wao.

Kocha huyo amesema mchezo huo unataorajiwa kuchezwa saa tatu usiku timu zote zinasaka pointi tatu ndani ya uwanja, watakuwa tayari kwa mchezo kesho.

“Wachezaji wanapata muda kidogo kati ya mchezo wetu uliopita na mchezo wa hivi karibuni tuliokuwa nao, unajua kila baada ya 48 moja na katika mchezo uliopita, tumefanya maandalizi mazuri na tupo tayari kukabiliana na Yanga,” amesema Moallin.

Mwakilishi wa wachezaji wa KMC FC, Daruweshi Saliboko amesema   kila kitu kimefanyiwa kazi na kocha amesahihisha makosa yaliyofanyika mechi zilizopita na kwenda kutafuta pointi muhimu mbele ya Yanga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button