Muziki

Kings Music nayo Oktoba 27, ya Zuchu na Nandy

DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya muziki ya Kings Music, inayoongozwa na msanii Ali Saleh Kiba maarufu Alikiba, imezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa ujumbe unaodokeza kuwa Novemba 27, mwaka huu, ni siku muhimu kwa kampuni hiyo.

Kupitia chapisho lake mitandaoni, Kings Music imeambatanisha ujumbe huo na maneno “OLEH OLEH (Official Release Date)”, jambo lililoibua udadisi miongoni mwa mashabiki wa muziki wanaojiuliza ni nini hasa kinatarajiwa kuachiwa siku hiyo.

Tangazo hilo limeibua tafsiri mbalimbali, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakilihusisha na mvutano wa kauli unaoendelea kuzungumziwa kati ya wasanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othuman maarufu Zuchu na Faustina Mfinanga, anayefahamika kama Nandy.

Tarehe hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee kutokana na mipango ya Nandy kuachia albamu yake mpya siku hiyo, huku pia ikiwa ni siku ambayo msanii Diamond Platnumz anatarajiwa kumfanyia sherehe ya siku ya kuzaliwa Zuchu.

Hali hiyo imeongeza udadisi kuhusu ujumbe wa Kings Music, hasa kutokana na muda wa tangazo hilo na matukio mengine ya kimuziki yanayotarajiwa kufanyika siku hiyo.

Hata hivyo, hadi sasa haijabainika rasmi iwapo ujumbe wa “Oleh Oleh” unahusiana na sakata hilo au ni sehemu ya maandalizi ya mradi mwingine wa muziki wa Kings Music.

Mashabiki sasa wanasubiri Novemba 27 ili kufahamu kile ambacho kampuni hiyo imewaandalia.

Related Articles

Back to top button