Muziki

Katy Perry kuchunguzwa

FILAMU ya msanii wa muziki Katy Perry wa nchini Marekani aliyorekodi kuzungumzia maisha yake huko Ibiza na Visiwa vya Balearic nchini Hispania inachunguzwa kwa uharibifu uliotajwa kuwa wa mazingira.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mazingira Asilia ya Visiwa vya Balearic, Agosti 13, imeeleza kuwa kampuni ya utayarishaji wa klipu hiyo “haikuwa imeomba idhini” ya kurekodi filamu.

Hati hiyo pia inadai shirika la mazingira limepokea taarifa nyingikuhusu ukiukaji unaodaiwa uliofanywa na kampuni ya uzalishaji wakati wa kupiga picha kwenye matuta ya mchanga ya S’Espalmador.

Video hiyo, iliyotolewa Agosti 8, iliongozwa na Stillz, mpiga picha na muongozaji wa filamu kutoka Colombia mwenye asili ya Marekani ambaye jina lake halisi ni Matias Vasquez.

“Hakuna idhini kampuni ya uzalishaji iliomba kutoka kwa Wizara kutekeleza upigaji picha, na ndiyo sababu hatua za uchunguzi wa awali zimeanzishwa,” ilieleza taarifa hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button