Ligi Kuu

JKT Tanzania yawatisha Simba

DAR ES SALAAM: JKT Tanzania imetuma salamu kwa wageni wao Simba SC, kuelekea mchezo utakaowakutanisha Jumamosi ya wiki hii ikieleza kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi kutokana na maandalizi mazito ambayo kikosi hicho imefanya.

Mchezo huo wa Ligi Kuu unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Msemaji wa JKT Masau Bwire, amesema timu yao ipo kwenye morali ya hali ya juu na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.

“Kwanza tunawakaribisha sana Simba. Lakini tunatoa pole za mapema kabisa kwao. Maana zile sare wanazopata wapinzani wao zimeisha. Kinachofuata ni kichapo cha kizalendo tu. Hapa Isamuhyo, mambo ni tofauti,” alisema.

Amesisitiza kuwa JKT haitacheza kwa presha ya majina bali kwa nidhamu ya kiufundi, umoja na malengo ya kupata ushindi muhimu kwenye uwanja wao wenye historia na uzalendo mkubwa.

“Hawa hawana chaguo zaidi ya kufungwa. Tumeshajiandaa, morali ipo juu, tunahitaji pointi na tunazichukua hapa kwetu,” aliongeza Bwire.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button