Muziki

Jaji Mkuu AGT, Simon Cowell kuomboleza kifo cha Payne kiaina

LONDON: JAJI Mkuu wa onesho la vipaji la American Got Talent (AGT), Simon Cowell amejiondoa kushiriki katika usahiri wa onesho la Britain’s Got Talent (BGT) la Uingereza kutokana na kifo cha kutisha cha mwanamuziki Liam Payne aliyejirusha kutoka ghorofani.

Liam Payne aliyekuwa nyota wa kundi la The One Direction, amefariki akiwa na miaka 31na kifo chake kilitokana na kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya jengo la hoteli katika mji mkuu wa Argentina akihusishwa kufanya hivyo baada ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe na matumizi ya dawa za kulevya.

Simon mwenye miaka 65, ameamua kupumzika tangu siku ya kifo cha mwanamuziki huyo na hatokuwa sehemu ya waandaaji wa kipindi cha Britan’s Got Talent cha Uingereza wiki hii na Jaji Bruno Tonioli atachukua nafasi yake.

Simon alionekana kwenye gari lake akiendeshwa na usalama wake, alifunika macho yake kwa vivuli vyeusi vya ‘Aviator’ huku akiwa na sura ya huzuni baada ya kutangazwa kufanya uamuzi wa kupumzika kwa muda kufuatia kifo cha Liam mwanamuziki ambaye ana mchango mkubwa mno katika muziki na kundi la One Direction.

Utayarishaji wa onesho hilo uliositishwa utaendelea siku ya Jumapili, lakini Simon hatakuwepo huku majaji wenzake Simon, Amanda Holden, Alesha Dixon, KSI na Bruno wataendelea kurekodi na majukumu ya kipindi hicho.

“Habari hizi zimemgusa sana Simon ambaye pia ni nguli katika kipindi cha X Factor, ameshtuka na amesikitishwa mno. Simon alimpenda Liam na alikuwa karibu na familia yake na lazima atakwenda kutoa pole,” mmoja wa watu wa karibu wa Simon alieleza.

Jaji mwingine wa kipindi hicho Nicole Scherzinger ndiye aliyekuwa nyuma ya kundi la muziki la One Direction na Simon alitoa msaada mkubwa kwa wasanii hao hadi walipofikia kimafanikio na jina la One Direction yeye ndiye aliwapa wasanii wa kundi hilo Liam, Louis Tomlinson, Niall Horan, Harry Styles na Zayn Malik.

Awali baada ya kifo cha mwanamuziki huyo Polisi, wazima moto na magari ya kubebea wagonjwa walionekana nje ya jengo la hoteli baada ya Liam kuanguka vibaya. Awali Polisi walifika baada ya kuripotiwa kuhusu mwanaume aliyekuwa akifanya fujo katika hoteli hiyo baada ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe, dawa za kulevya.

Related Articles

Back to top button