Filamu

Isarito: Tunahitaji waongozaji filamu kutoka nje

ZANZIBAR: MMOJA wa waigizaji wanaofanya vizuri katika Sanaa ya uigizaji wa filamu za mapigano nchini Tanzania, Isarito Mwakalindile amesema ujio wa Studio kubwa ya Idris Elba hautazuia kazi za Watanzania wala wazaznibar bali zitapandisha filamu na wasanii wan chi hizo mbili.

Mwakalindile ambaye anatamba na tamthilia ya Bunji akiwa na filamu yake mpya ya ‘My Son’ amesema wanachotakiwa sasa ni kuthubutu kwa kupitia uwekezaji wa Idris Elba wa studio hiyo kutawafanya wote wanaothubutu kuwa na nafasi kubwa zaidi katika soko la filamu.

Katika mahojiano baada ya kuonesha filamu yake ya My Son katika ukumbi wa wazi wa filamu wa Ngome Kongwe, amesema waigizaji na waongoza kutoka nje kwa kuwa wapo vizuri kartika uzalishaji wa filamu tofauti na ilivyo kwa tanzania.

Akizungumzia sekta ya filamu amesema kwamba anaona mwanga mkubwa kutokana na mafanikio ambayo anayapata katiika filamu ambazio ameshatengeneza.

Ameeleza kwamba siri ya mafanikio ni kukaza buti na kukamilisha mchakato wa kutengeneza sinema bila kulipua.

Mwakalindile pia alisema ni vyema watu wanaotengeneza sinema kutumia jukwaa kama la ZIFF ili kutanua wigo wa elimu na soko la filamu.

Related Articles

Back to top button