Tetesi

Inter yakataa bil 102/-za Man Utd kumsajili Onana

INTER Milan imekataa ofa ya kwanza kutoka kwa Mancheter United kwa ajili ya kumsajili golikipa Andre Onana.

United imebainisha Onana kama lengo kuu la golikipa na inatumaini kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon ingawa ina nia kutozidisha uthamini wao kwake.

Mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yanaendelea na kuna matumaini dili kufikiwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya michezo ya 90min, inaaminika ofa kutoka United ina thamani ya Euro milioni 40 sawa na shilingi bilioni 102 pamoja na nyongeza ya Euro milioni 5 sawa na shilingi 12.7.

Uthamini wa United kwa Onana ambaye alikuwa na kiwango bora msimu uliopita hasa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City ni Euro milioni 60 sawa na shilingi bilioni 153.1.

Man Utd inaona Onana ana thamani ya Euro milini 50 sawa na shilingi bilioni 127.59.

Onana anashinikiza kuondoka Inter na kama ilivyoripotiwa mapema wiki hii amekataa kusajiliwa Saudi Arabia akiwa na matumaini dili la kuhamia Ligi Kuu England litakamilika.

United inatarajiwa kuwa imara katika majadiliano kama ilivyoonesha kwa Chelsea kuhusu uhamisho wa Mason Mount ambao umethibitishwa Juni 5.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button