World Cup

Infantino aishutumu Magharibi kwa ‘unafiki’

RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) Gianni Infantino amezishutumu nchi za Magharibi kwa alichoita ‘unafiki’ katika ripoti ya nchi hizo kuhusu rekodi ya haki za binadamu ya Qatar iliyotolewa kuelekea fainali za Kombe la Dunia.

Katika hotuba ndefu isiyokuwa ya kawaida katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Qatar Infantino amezungumza kwa karibu saa 1 akiitetea Qatar na michuano hiyo.

Michuano hiyo imegubikwa na masuala kadhaa nchini Qatar yakiwemo madai ya vifo vya wafanyakazi wahamiaji.

Infantino mzaliwa wa Uswisi amesema mataifa ya Ulaya yanapaswa kuomba radhi kwa vitendo vilivyofanywa katika historia zao, badala ya kuzingatia masuala ya wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar.

“Leo nina hisia kali. Leo ninahisi Qatar, nahisi Mwarabu, nahisi Mwafrika, nahisi mlemavu, nahisi mfanyakazi mhamiaji,” amesema Infantino.

Uwanja wa Al Bayt utakaotumika katika ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia Qatar, 2022.

Mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2022 Qatar inafungua michuano hiyo Novemba 20 dhidi ya Ecuador katika uwanja wa Al Bayt uliopo mji wa Al Khor.

Related Articles

Back to top button