CHAN

Infantino aifuata fainali ya CHAN Nairobi

NAIROBI: RAIS wa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Gianni Infantino, anatarajiwa kushuhudia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Moi, Kasarani nchini Kenya Jumamosi ya Agosti 30 mwaka huu.

Infantino atashuhudia fainali hiyo ya Morocco na Madagascar sambamba viongozi wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) akiwemo Rais Patrice Motsepe, pamoja na marais wa mashirikisho 54 ya soka barani Afrika.

Viongozi wakuu wa serikali ya Kenya pia wanatarajiwa kuwepo uwanjani hapo wakiongozwa na Rais wa taifa hilo William Ruto, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, Naibu Rais Kithure Kindiki, Waziri wa Michezo Salim Mvurya na Rais wa Shirikisho la soka Kenya (FKF), Hussein Mohammed.

Tangu achaguliwe kuwa Rais wa FIFA, Infantino hajawahi kufika nchini Kenya, na hii itakuwa mara yake ya kwanza.

Kuhudhuria kwa Infantino kunachukuliwa kama ishara ya kuonesha imani na kuunga mkono uongozi wa soka nchini Kenya, hasa ikizingatiwa kwamba FKF imepita katika changamoto za uongozi zilizowahi kutishia mustakabali wa soka nchini humo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button